Kwa mujibu wa shirika la habari ABNA kwa kunukuu Al Jazeera, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, leo Jumatatu katika hotuba yake alidai: "Gaza haitajengwa upya mpaka Hamas na silaha zote zilizopo pale zitakapoangamizwa na itikadi kali kukomeshwa."
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kuhusu hili alidai: "Nataka muungano wetu na Marekani uendelee, lakini pia nataka tuwe huru katika silaha zetu. Sikubaliani na Rais Trump kuhusu Hamas; siamini kwamba tukijenga upya Gaza, asili yake itabadilika."
Hali ni hivyo wakati uchokozi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wanyonge na wasio na ulinzi wa Gaza kwa amri ya moja kwa moja ya Netanyahu hadi sasa umeacha makumi ya maelfu ya mashahidi.
Maoni yako